Tembelea... |
 |
Kalenda |
 |

Marafiki wetu |
 |
Habari Zilizopita |
 |



  
| |
 |
|
|
 |
 |
|
HII NDIYO ZAWADI YAKO MSOMAJI!
|
photos |
|
|
 |
Hadi sasa, wewe msomaji, umetembelea mtandao huu zaidi ya MILIONI 4! Na umetembelea ndani ya kipindi kisichozidi miezi 17 kuanzia SEPTEMBER 2007. Tunakushukuru na kukupongeza sana. Hatuna jambo kubwa la kufanya kuonesha shukrani yetu itakayolingana na umuhimu wako. Wakati tunaelekea kutimiza msomaji wa MILIONI 5, tumetenga zawadi ya simu aina ya BLACKBERRY 8700G. Zawadi hii utaipata ukibahatika kuangukia nambari 5000000 (milioni 5) siku utakapofungua website hii (Angalia counter mwisho wa page hii, kona ya kushoto). Utakachotakiwa kufanya ni kuprint screen popote ulipo duniani na kututumia kama ushahidi kwa email: uwazi@hotmail.com. (tafadhali usifanye usanii, utaumbuka).
MBALI YA ZAWADI HIYO, wewe kama ni mkazi wa Dar es salaam, ukisoma tangazo hii, nenda duka maarufu linalouza VIPODOZI, HAND BAGS na VIATU kutoka Marekani, ARISE BEAUTY SUPPLY, jitambulishe kuwa umeona tangazo hili kwenye mtandao wa Global Publishers na utapewa PUNGUZO LA ASILIMIA 20 kwa bidhaa yoyote utakayoinunua katika kipindi hiki. ARISE BEAUTY SUPPLY, wapo Mikocheni B, jirani na klabu ya Talk of The Town na Sinza Mapambano, bidhaa zao ni HIGH QUALITY FROM USA na Brands zao ni pamoja na Victoria's Secret, Avon, LA Girl, n.k. Hawa ndiyo wadhamini wetu, ongea nao zaidi kwa namba: +255 784 521171, +255 784 456046 (MIKOCHENI) na +255 0753 335011 (SINZA). Au tembelea mtandao wao:WWW.ARISE-TZ.COM
 (soma zaidi kuona baadhi ya bidhaa zao) |
|
 |

 |
|
 |
MTIKILA AJISALIMISHA KORTINI Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha Democratic Part (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, leo amejisalimisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, baada ya mahakama hiyo kuamuru akametwe kutokana na kutofika kusikiliza kesi yake jana. Mtikila aliueleza mtandao wetu mahakamani hapo, kuwa alifika kwaajili ya kuwasilisha hati yake ya kuiomba radhi mahakama hiyo.Pichani Mtikila (mwenye tai) akiongea na baadhi ya mapaparazi mapema hii leo, baada ya kujisalimisha mahakamani hapo. HATIMA YA OMBI LA MRAMBA KUSAFIRI NJE YA DAR KUSHUGHULIKIWA Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Da es Salaam, imesema kuwa inaendelea kushughulikia ombi la aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Pesambili Mramba la kusafiri nje ya mkoa wa Dar. Hakimu anayesikiliza kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kulisababishia Taifa hasara ya zaidi ya Sh.Bilioni 11 inayowakabili Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona, pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wizara hiyo Grey Mgonja, Hezron Mwankenja, ameuambia mtandao huu mapema hii leo kuwa suala hilo huenda likafafanuliwa vizuri Januari 7. Mramba aliiomba mahakama hiyo hivi karibuni ili iweze kumpa kibari cha kwenda kuwasalimia wapiga kura wake. MATAA YA UMEME WA JUA KUANZA KUTUMIKA DAR Jiji la Dar es Salaam huenda likaondokana na kero ya mataa ya kuongozea magari, kutokana na kuanza kufunga kwa mataa hayo yanayotumia nguvu za Jua.Mtandao huu umeshuhudia nguzo nyingi za mataa hayo, zikiwa zimeandaliwa kama inavyoonekana pichani katika makutano ya Barabara za Shekilango na Bagamoyo Jijini Dar. SPORTS KILIMANJARO STARS KUMENYANA NA WANDA KESHO Baada ya kufufua matumaini yake katika michuano ya Kombe la Chalenji kwa kuilaza timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa mabao 2-1,timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kesho inatarajia kushuka tena dimba la Nakivubo nchini Uganda, kukwaruzana na timu ya Taifa ya Rwanda. Kilimanjaro Stars, wanaonolewa na Mbrazil Marcio Maximo, wanatarajia kushuka dimbani hilo wakitaka kupata pointi tatu muhimu, ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali. KIBONZO  PICHA ZOTE NA CHRISTOPHE LISSA/GPL |
|
 |
 |
|
 |
Muddy, mlemavu ambaye si rahisi kumgundua kuwa ni muuaji kutokana na alivyoonekana machoni mwa wananchi analisumbua Jeshi la Polisi kwa kipindi kirefu, kazi yake kubwa ni kuua wanawake na kuwakata sehemu zao za siri kisha kuwagonga muhuri wenye alama ya 10000DY! Kazi ambayo ana ndoto kubwa ya kujipatia utajiri baada ya kumuuzia mganga wa kienyeji mwenyeji wa Zambia kwa ajili ya mambo ya kishirikina, wakiamini viungo hivyo hufanya migodi itoe dhahabu nyingi.
Baada ya kufanikiwa kuwatoroka askari hatimaye Muddy anapata lift ya Fuso akijifanya mwanafunzi nia yake atoke katikati ya Jiji la Dar es Salaam anapotafutwa kwa udi na uvumba, hata hivyo ndani ya Fuso alipowekwa nyuma ya bodi inasikika harufu kali sana, mwisho anajitetea kuwa ni dawa ya tumbo aliyoiweka.
Askari wanaamua kumfuatilia muuaji huyo na kuweka geti kila njia inayotoka jijini ili kukagua magari ya abiria na mizigo wakimtafuta Muddy. Ndani ya Fuso alipokuwa Muddy dereva anaulizwa na askari iwapo amebeba abiria mlemavu, bila kuficha kutokana na maelezo ya askari anafichua siri kuwa amebeba mlemavu mwenye mfuko unaotoa harufu kali, zoezi la kumtia mikononi Muddy linakuwa rahisi, wanamfikisha Kituo cha Polisi Kibaha na baadaye akasafirishwa mpaka jijini Dar es Salaam, wakuu wote wa jeshi hilo pamoja na Inspekta Jenerali anamshuhudia Muddy aliyekuwa akiwanyima usingizi. Anapigwa hali inayomfanya aombe kuelezea kilichotokea. Je, Muddy anataka kuwaeleza nini askari? SONGA NAYO... |
|
 |
 |
|
NGELEJA ALINGIA MAFANIKIO WIZARA YA NISHATI NA MADINI
|
photos |
|
|
 |
Waziri wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja (MB), amesema kuwa wizara yake imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005-2008 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mapema hii leo, katika ukumbi wa wizara yake, Ngeleja alibainisha maeneo ambayo wizara hiyo imeweza kupata mafanikio makubwa kuwa ni pamoja na Sekta ya Nishati na Madini. Ngeleja alisema kuwa, kwa mwaka 2007 sekta ya Nishati (selta ndogo ya umeme asilia) ilikua kwa asilimia 10.9 ikilinganishwa na asilimia 9.0 ya mwaka 2005. "Mwaka 2007 umeme uliozalishwa ulikuwa ‘megawatt/hour’ (MWh) 4,204.62 ikilinganishwa na MWh 3,148.85 kwa mwaka 2005"alisema Ngeleja. Aidha, waziri huyo alisema kuwa Sekta ya Madini ilikua kwa asilimia 16.1 mwaka 2005, asilimia 15.6 mwaka 2006 na asilimia 2.7 mwaka 2007. "Mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa uliongezeka kutoka asilimia 2.4 mwaka 2005 hadi asilimia 2.7 mwaka 2007"alibainisha Waziri huyo. PICHA NA CHRISTOPHER LISSA NA RICHARD BUKOS/GPL |
|
 |
|
|
 |
Kura Yako / Poll |
 |
Habari Katika Picha |
|
 |

Nani Yupo / Alikuwepo |
 |
|